MIAKA MINNE YA RAIS DKT. SAMIA IMEPAISHA DIPLOMASIA YA NCHI KIUCHUMI - MBUNGE BALOZI MULAMULA


 ****

MBUNGE Balozi Liberata Mulamula, amempongeza kwa dhati Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kutimiza miaka minne madarakani tangu kuapishwa Machi 19, 2021.

Balozi Mulamula ameyasema hayo, alipozungumzia mafanikio ya Rais Dk. Samia katika miaka minne hususan upande wa diplomasia.

"Kwa dhati ya moyo wangu, nampongeza mwana diplomasia namba moja kwa kuipaisha diplomasia yetu ya uchumi kwa maono yake na wepesi katika kujenga na kukuza mahusiano yetu na nchi za nje duniani na mashirika ya kimataifa.

"Hii ni pamoja na kuhamasisha wawekezaji na misaada mbalimbali ya kuinua uchumi wetu na ustawi wa jamii na taifa letu kwa ujumla katika nyanja mbali mbali," alisema.

Aidha, alimpongeza Rais Dkt. Samia kwa kuvutia mikutano mikubwa ya kimataifa kufanyika nchini kipindi hiki ambacho imehudhuriwa na Wakuu wa Nchi wa kanda ya Afrika na kwingine duniani, huku Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wakifika nchini ni kielelezo tosha cha ukuaji wa diplomasia yetu ya uchumi na uongozi wake kutambulika na kukubalika ulimwenguni kote. 


00000000

0/Post a Comment/Comments