NEMC YATEKETEZA TANI 150 YA VIFUNGASHIO


............................

Baraza la Taifa la hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limesajili jumla ya miradi 8,058, ambapo kati ya hiyo, 5,784 ni ya tathmini ya Athari kwa Mazingira. 

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu Baraza hilo Dkt. Emmaculate Swali wakati akielezea mafanikio na muelekeo wa baraza hilo ndani ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita Leo machi 23,2025 jijini Dodoma.

Aidha ameeleza kuwa Baraza hilo limefanikiwa kuandaa vipindi 88 vya uhamasishaji kupitia vyombo vya habari na mikutano 20 ya wadau kuhusu madhara ya matumizi ya mifuko ya plastiki. 

Vilevile, amesema kaguzi zilifanyika katika maeneo 178 ya uzalishaji na usambazaji wa mifuko ya plastiki, ambapo maeneo 57 yalikutwa na makosa na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria.

 Zaidi ya Tani 150 za vifungashio visivyokidhi viwango vilikamatwa, vikataifishwa na kuteketezwa kwa mujibu wa Sheria hata hivyo suala la udhibi wa vifungashio vya plastiki ni letu Sote.

Baraza hilo linaendelea kusimamia utekelezaji wa majukumu yake wa kizazi cha sasa na baadae.

0/Post a Comment/Comments