NGORONGORO YAFANIKIWA KUDHIBITI UJANGILI

  ****

Na Ester Maile....Dodoma

Katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia suluhu hassan Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Imedhibiti ujangili wa wanyamapori ndani na nje ya hifadhi kwa kushirikiana na vikosi maalum na vyombo vya usalama .

Ameyaeleza haya Kamishina wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Dkt Elirehema Doliye,wakati akizungumza na waandishi wa habari leo march 10 jijini Dodoma akieleza mafanikio katika mamlaka hiyo.

Pia kupungua kwa ujangili wa tembo yamepungua kutoka 25 mwaka 2020-2021 hadi kufikia tukio moja kwa 2022-2023 na 2024 hakuna tukio lililotokea .

Kumeongezeka kwa idadi kubwa ya wanyamapori idadi ya faru weusi waongezeka kwa asilimia 40 kutoka mwaka 2020 hadi 2024,pia idadi ya simba nimefikia 188. Na tembo imeongezeka kutoka 800 mwaka 2020 hadi makadirio ya 1300 kwa mwaka 2024.





 

0/Post a Comment/Comments