NSSF YATATUA CHANGAMOTO KATIKA MIRADI YA UWEKEZAJI


****

Na Ester Maile .....Dodoma 

Mfumo wa Taifa wa hifadhi jamii imefanikiwa kutatua changamoto zilizokuwa zinakabili miradi ya ujenzi na kusababisha miradi ya Dungu,Toangoma kijichi iii,Mzizima na Hoteli ya kitalii Mwanza kusimama kati ya mwaka 2016_2021 kupisha zoezi la ukaguzi maalum.

Ameyaeleza hayo Mkurugenzi wa mfuko wa Taifa wa hifadhi jamii Masha Mshomba kwenye mkutano wake na waandishi wa habari leo 17 march 2025 jijini Dodoma.akizungumzia mafanikio ya NSSF kwa kipindi cha miaka minne cha uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan. 

Masha amesema utatuzi uliofanyika unahusisha kupatikana kwa mwendesha Hoteli kawa ajili ya miradi ya Mzizima na Hoteli ya kitalii Mwanza.

Pamoja na kutatua changamotoza mikataba ya wakandarasi waliotelekeza miradi ya Dungu,Toangoma na Kijichi iii, sasa miradi yote hiyo inaendelea na kutarajiwa kukamilika kati ya juni 2025 hadi juni 2026.

Hata hivyo mfuko wa Taifa wa hifadhi jamii inampango wa kuendelea kutekeleza mikakati ya ukuaji wa mfuko ilikufikia thamani ya shilingi trilioni 11000.00 mwezi wa juni 2026 ni mara mbili ya thamani ya shilingi trilion 5068.82 iliyofikia mwezi juni 2021.

Mwisho Nssf imeimalisha mifuko na matumizi ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi na kupunguza malalamiko kwa wanachama wake.



 

0/Post a Comment/Comments