MBETO ASEMA WALICHOKIPAMDA ACT WAZALENDO NDICHO WATAKIVUNA


 ::::::::::

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimekitaka ACT Wazalendo kisimtafute mchawi katika sakata la kuenguliwa mgombea wao wa urais , badala yake wajue kinachopandwa ndicho kinachovunwa.

Pia kimemtaka Kiongozi Mstaafu wa chama hicho Zito Kabwe kuacha kutoa shutuma zisozo na sababu wakati Luhaga Mpina ameengulia kwa kukiuka masharti ya katiba ya chama hicho.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis ameeleza hayo na kusema yaliowakuta ni matokeo ya dhulma aliofanyiwa Kiogozi wa chama hicho Doroth Semu kwa kulazimishwa ajitoe kuwania Urais .

Mbeto alisema tayari ACT walishateua jina la mgombea wa urais lakini kutokana na mizengwe ya viongozi watatu wa chama ndiko kulikoleta kizaazaa chote

Aliwataja viongozi hao ni Makamu Mwenyekiti ACT Wazalendo Ismail Jussa Ladhu ,Mwanasheria wao Ramadhan Said Shaaban na Zito Kabwe ndio waliosabisha yotekee yalitokea

"Vigogo watatu wa ACT Wazalendo wamehusika kuvunja katiba ya chama hicho. Walidhani wanachama ni mbumbumbu wa Katiba. Kuvunja katiba kwa maslahi binafsi ni zaidi ya udikteta " Alisema Mbeto 

Aidha, Mbeto alimtaka Zitto awe mkweli kwa kukosea na kuacha kuitupia lawama CCM wakati anajua fika waliokitosa chama hicho kikose mgombea urais ni yeye na wenzake .

"ACT kiache upotoshaji . Zito anapodai CCM imemzuia Luhaga Mpina ni madai ya kitoto na kipuuzi .Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoanj wa Arusha Dk Godfrey Malisa ameshitaki Mahakama Kuu .Je ametumwa na Zito au Jussa "Alihoji Mwenezi huyo .

Mbeto amekitaka ACT hicho kwanza kuheshimu matakwa ya katiba yake ,kifuate taratibu na kikanuni bila kuamua mambo kwa mihemko au kwa upendeleo .

"Hii ni mara ya Pili viongozi wa ACT wanafanya maamuzi kwa pupa na batili .Mwaka 2020 kilimdandia Marehemu Bernad Membe na kumtaka awanie urais kisha vigogo wa ACT wakagoma kumfanyia kampeni" Alikumbusha

Hata hivyo Mbeto alihoji sababu za kuliondoa jina la Dorothy ambaye alipitishwa na mkutano Mkuu wa Taifa wa ACT kama ambavyo mgombea urais wa CCM Rais Dk Samia Suluhu Hassan alivyoidhinishwa

"Jussa na Zito ni madikteta uchwara wasiothamini Usawa wa Kijinsia . Wametumia ubabe kuliondoa jina la mgombea halali ili kumpandikiza mgombea asiyekidhi matakwa ya katiba pia akiwa hana sifa ya uanachama wake " Alisisitiza Mbeto

0/Post a Comment/Comments