POLISI-KISIJU NI SALAMA

..........

Jeshi la Polisi Tanzania limewataka wananchi kuendelea kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu na kuwahakikishia kuwa nchi ipo salama

Polisi wamesema wanaendelea kufuatilia tahadhari ya uwepo wa tishio la kiusalama katika maeneo ya ukanda wa Pwani nchini, hususani maeneo ya kusini mwa Kisiju

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi leo March 22,2025 imesema “March 21, 2025 kupitia mitandao ya kijamii ilitolewa taarifa inayotoa tahadhari juu ya uwepo wa tishio la kiusalama katika maeneo ya ukanda wa Pwani hapa chini hususan maeneo ya Kusini mwa Kisiju, tunafuatilia suala hilo"

March 21,2025 Ubalozi wa Marekani ulitoa tahadhari ya kiusalama na kuwataka Raia wa Marekani wajiepushe kutembelea maeneo ya visiwani na maeneo ya pwani hususani kusini mwa Kisiju. 

0/Post a Comment/Comments