RAIS DK.SAMIA AIPONGEZA ORYX GAS KAMPENI NISHATI SAFI YA KUPIKIA

*****

Na Mwandishi Wetu,Muheza

RAIS DK.Samia Suluhu Hassan amekutana na 

Oryx Gas pamoja na wadau wengine ambapo wamemuhakikishia wataendelea kuunga mkono kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kupeleka mitungi ya gesi vijijini ili kuwezesha wananchi kuipata kwa urahisi.

Ametoa kauli hiyo alipotembelea banda la Oryx Gas wakati wa uzinduzi wa kampeni ya matumizi  nishati safi ya kupikia Kitaifa iliyozinduliwa katika viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza mkoani Tanga.

"Mitungi ya gesi inapoisha inabaki ndani kama feniture (Samani za ndani) ,hivyo nimeomba sekta binafsi na  nimekutana na Oryx Gas na wadau wengine na wakanihakikishia  wataendelea kuipeleka mitungi  ili wananchi waendelee kutumia.”amesema Rais Samia huku akiipongeza Oryx Gas.

Awali akitoa maelezo kwa Rais Samia, Meneja Miradi ya Nishati Safi ya Kupikia kutoka Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba amesema kampuni hiyo imekuwa ikifanya jitihada mbambali za kuunga mkono kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini na mkakati wao ni kuona kila nyumba inakuwa na mtungi wa gesi ya kupikia.

“Tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa ajenda yake ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Oryx Gas tumekuwa wadau wakubwa na tumefanya jitihada nyingi tokeo ilipotangazwa kama ajenda rasmi ya nchi kwamba wananchi tuanze kutumia nishati safi ya kupikia 

“Tumeongeza miundombinu ya kusambaza mitungi ya Oryx Gas hasa katika maeneo ya vijiji ambapo kwa sasa huwezi kuikosa Oryx gas. mitungi ya Oryx inapatikana kila miji,Wilaya na vijijini pia tupo .Pia tumekuwa tukishiriki katika shughuli za mbalimbali za kuwezesha ukuaji wa matumizi ya nishati safi  ambapo tumeweza kuisaidia  jamii mbalimbali ikiwemo ya Wanawake kwa kuiwezesha kufikia hayo malengo.








 

0/Post a Comment/Comments