Rais wa Marekani, Donald Trump ameamuru kufungwa kwa muda Kituo cha Habari cha Sauti ya Amerika (VOA).
Hatua hiyo imesababisha zaidi ya wafanyakazi 1,300 kwenda likizo ya lazima.
Uamuzi wa Trump umeyaathiri pia mashirika sita ya habari yanayofadhiliwa na Serikali ya shirikisho ikiwa ni pamoja na Redio Free Europe na Redio Free Asia.
Mkurugenzi wa VOA ambayo hutangaza kwa karibu lugha 50, Michael Abramowitz ameeleza kusikitishwa na uamuzi huo, akisema hii ni mara ya kwanza baada ya miaka 83 Sauti ya Amerika inazimwa.
Amesema VOA imekuwa na jukumu muhimu katika kupigania uhuru na demokrasia kote duniani, na kwamba uamuzi wa Trump unakiathiri chombo hicho ambacho hutumika kama chanzo cha habari za kuaminika katika mataifa mbalimbali.
Shirika la kimataifa la waandishi wa habari wasiokuwa na mipaka limelaani uamuzi huo wa Rais Trump na kulitaka Bunge la Marekani na Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua dhidi ya uamuzi huo ambao haujawahi kushuhudiwa.
VOA ilianzishwa mwaka 1942 ili kukabiliana na propaganda za Wanazi wa Ujerumani na huwafikia karibu watu milioni 360 kwa wiki.
Post a Comment