SACP PASUA AWAONGOZA MAOFISA WA POLISI KUKAGUA MRADI WA UFUGAJI WA CAMERA ZA BARABARANI LONGIDO

***

Na Mwandishi Jeshi la Polisi Longido Arusha.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Simon Pasua amewaongoza maafisa wa Polisi Mkoa wa Arusha kutembelea na kuona mradi wa ufungaji kamera za Barabarani wilayani Longido Mkoani Arusha

Akiwa katika mradi huo SACP Pasua amesema mradi huo umelenga kusaidia na kubaini vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu huku akiwaomba wananchi kuupokea na kuulinda mradi huo ambao utasaidia kudhibiti uhalifu.

Aidha amelipongeza shirika la OIKOS linalofadhili mradi huo ambapo amesema mradi huo utakapo kamilika utasaidia kukabiliana na vitendo vya uhalifu na kumaliza changamoto ya vitendo vya uhalifu.

Sambamba na hayo pia ameweka wazi pia wafugaji nao watanufaika katika mradi huo ambapo utakomesha wizi na wa mifugo.







 

0/Post a Comment/Comments