Na Tausi Mbowe
Mwaka 2003 Serikali ilianzisha Mamlaka ya Chakula Dawa na Vipodozi (TFDA).
TFDA ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria Chakula Dawa na Vipodozi Sura Na. 219.
Kuanzishwa kwa mamlaka hiyo kulisaidia udhibiti na usimamizi wa dawa, chakula na vipodozi jukumu ambalo ililifanya kwa ufanisi mkubwa hadi pale Seikali kupitia Wizara ya Afya ilipofanya mabadiliko na kuondoa maadhi ya majukumu na kupeleka katika mamlaka nyingine ikiwako Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Pamoja na mambo mengine TFDA ilianzisha mambo mbalimbali ikiwamo Uanzishwaji wa Maabara wa Maabara jijini katika ofisi za Dar es Salaam, Uanzishwaji wa mpango wa maduka muhimu pamoja na uanzishwaji wa ofisi kanda ya Ziwa Mwanza.
Pia ilifanya ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la. makao makuu jijini Dar es Salaam na kuanza kazi.
*Kubadilika kwa jina kutoka TFDA kwenda TMDA*
Mwaka 2019 Serikali ilibadili jina la Mamalaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) na kuwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA).
Mabadiliko hayo yalifuatia marekebsho ya Sheria ya Dawa Chakula na Vipodozi Sura Na. 219 kupitia Sheria ya Fedha Na. 8 ya mwaka 2019.
Mbali na kubadili njina la sheria hiyo kuwa Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba sura ya 219 pia ilihamisha majukumu ya kudhibiti ubora na usalama wa chakula na vipodozi kwenda katika sheria ya Viwango Sura ya 130 ambayo iko chini ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Kwa sasa TMDA ndiyo msimamizi mkuu wa Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi jukuku ambalo inalitekeleza kwa ufanisi mkuu.
TMDA imeweka mifumo mbalimbali, kuboresha maabara zake ili kudhibiti uingizwaji holela wa dawa na vifaa tiba zisizo na ubora lakn pia kuboresha kitengo chake cha habari kwa lengo la kutoa elimu na kuwafikia wananchi zaidi.
Post a Comment