****
Saudi Arabia imetangaza Jumapili, Machi 30 kuwa sikukuu ya Eid al-Fitr baada ya mwezi mwandamo wa Shawwal, mwezi wa kumi katika kalenda ya Kiislamu kuonekana.
Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) na Qatar pia zimethibitisha kuwa Eid al-Fitr itakuwa Jumapili. Hata hivyo, Oman na Iran zimetangaza kuwa Eid al-Fitr kwao itaanza Jumatatu, Machi 31, 2025.
Post a Comment