Wizara ya Afya imethibitisha kesi mbili za ugonjwa wa Mpox nchini Tanzania baada ya uchunguzi wa maabara kufanyika kwa wahisiwa.
Kesi hizi zilipatikana kwa wagonjwa waliokuwa na dalili kama vile homa, vidonda kwenye ngozi, maumivu ya viungo, na vipele.
Aidha, Wizara imetoa taarifa kuhusu ugonjwa wa Marburg, ikieleza kuwa kwa siku 41 zilizopita hakuna mgonjwa mpya aliyeripotiwa, ikimaanisha kuwa udhibiti wa ugonjwa huu unaendelea vyema.
Wananchi wanashauriwa kuchukua tahadhari na kuripoti dalili zozote za Mpox kwa kupiga simu 199 bila malipo.
Serikali inachukua hatua madhubuti kudhibiti maambukizi kwa kufuatilia wahisiwa wengine na kutoa elimu kwa umma juu ya njia za kujikinga. Wananchi wanahimizwa kuepuka kugusana moja kwa moja na wagonjwa, kutumia vifaa binafsi, na kunawa mikono mara kwa mara.
Post a Comment