*****
SERIKALI ya Cuba imesema ushirikiano wake na Tanzania ni wa kihistoria na itaendelea kudumisha uhusiano huo kwa faida ya nchi hizo.
Hayo yamesemwa leo mapema kibaha mkoani pwani na Rais wa Baraza la Taifa na Bunge la Jamhuri ya Cuba, Mhe. Esteban Lazo Hernandez,wakati alipokuwa akitembelea KIWANDA cha Kibaiolojia cha Tanzania Biotech Product limited (TBPL) kilichopo mkoani hapa kwa lengo la kuangalia utendaji wake.
"Uhusiano wa Cuba ni wa siku nyingi toka uhuru na mahusiano yaliojengwa na kuhasisiwa viongozi wetu akiwemo Rais wa zamani wa Cuba,
Fidel Castro na Marehemu Julius Kambarage Nyerere"amesema
Hernandez amesema kutokana uhusiano huo umepelekea kuwepo kiwanda cha TBPL ni sehemu ni teknolojia ambayo inapatikana nchini Cuba na kusema kimesaidia kupambana vita dhidi ya Ugonjwa wa Malaria"
Amesema kutokana uwekezaji wa nchi hizo mbili kwa sasa wanafanyia kazi uzalishaji na kupelekea kuzalisha lita milioni sita za viwadudu na viwatilifu hai.
"Hivi karibuni kitaanza kutengeneza Mbolea hai na pia kitaanza kutengeneza bidhaa kumi,na umuhimu wa kiwanda umetokana na sera za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassani katika mapambano ya vita dhidi ya Maralia"Amesema
Kwa upande wake ,Balozi wa Tanzania nchini Cuba,Hamprey Polepole,ametoa Rai kwa Halmashauri zinapokewa Viwadudu kupuliza kwa utaalamu kwenye maeneo yao ili kukabiliana na ugonjwa Malaria.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara,Dkt. Suleiman Hassan Serera.Amesema kiwanda hicho kuzalisha lita milioni moja na kwasasa hatua iliyopo ni kuitafutia soko kiwanda hicho.
Amesema lengo la wizara hiyo ni kuzalisha lita milioni sita na kutoa rai kwa watanzania kutumia bidhaa za kiwanda hicho.
Naye pia, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC)Dkt Dk Nicolaus Shombe,amesema kiwanda kinawataalamu kutoka Cuba na wanashirikiana katika uendeshaji.
Dkt Shombe amesema kwa mwaka huu serikali imeshatoa bilioni 4 kwa ajili ya Halmashauri mbalimbali nchini kwa ajili ya viwadudu.
"Kwa sasa tunauza nchi nane hapa Barani afrika lengo letu ni kutafuta masoko mengi"
Post a Comment