*****
Na mwandishi wetu Dar es salaam
Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB) imesema kuwa itaendelea kuwa mdau muhimu katika kuimarisha uchumi wa
mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla kupitia sekta mbalimbali za kijamii na
kiuchumi nchini.
*****
Akzingumza Katika hafla ya Iftari iliyofanyika leo Machi 28, 2025 jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Adam Mihayo, ameeleza dhamira ya benki hiyo kuwa ni kushirikiana na Serikali katika kujenga uchumi
imara.
Mihayo amesema kuwa benki hiyo imekuwa ikitoa misaada katika
sekta muhimu, ikiwemo kusaidia madawati katika shule na kutoa misaada katika
hospitali.
Ameongeza kuwa TCB inaendelea kupunguza mzigo kwa serikali
kwa kugusa moja kwa moja sekta zinazohitaji msaada na pia kuimarisha maendeleo
jumuishi kwa jamii.
Kwa uapnde wake Naibu Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Hassan
Chizenga, ameipongeza TCB kwa kuandaa tukio hilo lililoweka pamoja watu kutoka
makundi mbalimbali ya jamii, akisema kuwa hiyo ni mfano mzuri wa kujali na
kuungana kwa jamii.
Amesema kuwa benki
hiyo inapaswa kuendelea kuigusa jamii kwa vitendo, na kuonesha kwa mfano wake
ukongwe na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kijamii.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini, watoto kutoka vituo vya kulea watoto yatima, wafanyakazi wa TCB, wateja wa benki hiyo, na jumuiya ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism), ikiwa ni sehemu ya juhudi za TCB kuimarisha maendeleo jumuishi na kusaidia makundi yenye uhitaji.
Post a Comment