TEN/MET NA LHRC WATAKA KUFUTWA KWA ADHABU ZA VIBOKO SHULENI

 

******

Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wameibua mjadala kuhusiana na kufutwa kwa adhabu ya viboko shuleni. Mjadala huo umeibuka hivi karibuni baada ya kuripotiwa kifo cha mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari MWASAMBA mkoani SIMIYU, ambacho kinatajwa kimetokana na adhabu ya viboko iliyotolewa na Mwalimu wake.

Mratibu wa TENMET Kitaifa, MARTHA MAKALA, amesema watu wengi wanafikiri kwamba kutokana na mazingira yalivyo katika shule zetu, ni vigumu kuondoa adhabu ya viboko, ingawa kwenye maboresho ya sheria ya elimu kunasisitizwa kuondolewa kwa mustakabali wa ulinzi na usalama wa mwanafunzi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Wakili FULGANCE MASSAWE, ameiomba Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kutoa waraka unaozuia walimu kuacha matumizi ya viboko wakati mchakato wa marekebisho ya sheria ya elimu unaendelea.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji LHRC, Neema Kitundu, mwanachama wa TENMET, amesema pamoja na serikali kutoa miongozo ya namna ya kutoa adhabu, bado kuna changamoto kwa baadhi ya walimu katika utekelezaji wa adhabu ya viboko kwani uchapaji hauko sawa.





0/Post a Comment/Comments