..........................
Na Ester Maile.....Dodoma
Mamlaka ya Udhibiti wa MboleaTanzania (TFRA) imeboresha ukuaji wa biashara ya mbolea nchini ambapo wafanyabiashara wa mbolea waliopewa leseni wameongezeka kutoka 3,069 mwaka 2020_2021 hadi kufikia 7,302 Februari 2025
Ameyasema hayo Mkurugezi mtendaji wa Mamlaka hiyo Joel Laurent wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo 19 march 2025 akielezea mafanikio ya Mamlaka hiyo ndani ya miaka minne chini ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha amesema kuwa upatikanajia wa mbolea umeongezeka kutoka tani 766,024 mwaka 2020-2021 hadi tani 1213,729 mwaka 2023_2024 uingizaji wa mbolea umeongezeka kutoka tan 504122 hadi tani 728758 mwaka 2023_2024 vile vile uzalishaji wa ndani umeongezeka kutoka tani 42695 hadi tani 158628 mwaka 2023 _2024.
Pia kuboreshwa kwa mazingira ya uwekezaji nchini serikali imeongezeka viwanda vya mbolea kutoka viwanda 16 mwaka 2020-2021 hadi viwanda 33 mwaka 2023_2024 na kati ya viwanda hivyo vitatu ni viwanda vikubwa kumi na moja ni viwanda vya kati na tisa viwanda vidogo.
Hata hivyo Mamlaka ya Udhibiti wa MboleaTanzania (TFRA) imejipanga kuimarisha mifumo ya usambazaji wa mbolea ili kuhakikisha mbolea zinawafikia wakulima kwa wakati na kwa gharama nafuu.
Pia imesema inaendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya mbolea kwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya ili kuongeza matumizi ya mbolea.
Post a Comment