Na Tausi Mbowe
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), imeendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa na madhara yake iwapo zitatumika kiholela.
Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt Adam Fimbo ametoa elimu hiyo kwa wananchi walitembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonyesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendele jijini Dar es Salaam.
Dk Fimbo amesema, Mamlaka hiyo inaendelea kupambana na usugu wa vimelea vya dawa unaotokana na wagonjwa kutumoa dawa kiholela bila maelekezo ya wataalam wa afya.
"Usugu wa dawa umekuwa ukiongezeka siku hadi siku kutokana na matumizi yasiyo sahihi na holela bila kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya jambo linalo sababisha madhara makubwa kwa jamiii., " alisisitiza Dk Fimbo.
Kwa mujibu wa Dk Fimbo, TMDA imeshiriki maonyesho hayo ili kutoa elimu na kuwafikia wanachi wengi zaidi wanaofika katika viwanja hivyo.
Dkt Fimbo ametoa wito kwa wananhi wa jijini Dar es Salaam na mikoa ya jirani wanaofika katika maonyesho hayo kutembelea katika banda la TMDA ili kupata elimu zaidi ya matumizi sahihi ya dawa, vifaa tiba, vitendanishi pamoja na shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo.

Post a Comment