Na Tausi Mbowe
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) imeibuka kidedea katika Tuzo za Umahiri katika kampeni bora ya utoaji elimu kwa jamii.
TMDA imenyakuwa Tuzo hiyo usiku wa kuamkoa leo, Machi 29,2025 jijini Dar es Salaam.
Tuzo hizo zimezotolewa na Chama cha Maafisa Habari (PRST).
Akipokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Mamlaka hiyo, Meneja Uhusiano wa Umma, Gaudensia Simwanza alisema Tuzo hiyo ni heshima kwao kuendelea kufanya kazi kwa bidii kuwahudumia wananchi.
Kwa mujibu wa Simwanza Tuzo hiyo ni kielelezo cha kutoa huduma bora katika sekta ya afya na kuahidi kuendelea kuwafikia wananchi wengi zaidi.
"TMDA tutaendelea kuhakiiisha Watanzania wanapata huduma bora kwa kusimamia dawa, vifaa tiba na vitendanishi vinavyozingatia viwango vilivyoweka. "
Post a Comment