UCHAGUZI JUKWAA LA WAHARIRI WAPAMBA MOTO

.............

Ikiwa zimebaki siku 15 kabla ya kufanyika uchaguzi wa viongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ambaye ni mwenyekiti wa sasa, leo tarehe 21 Machi 2025 amechukua fomu kutetea nafasi hiyo.

Balile alisindikizwa kuchukua fomu ya kugombea na baadhi ya wanachama wa chama hicho.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 5 Aprili, 2025 mjini Songea mkoani Ruvuma ambapo utatanguliwa na Mkutano Maalum utakaoanza tarehe 3 Aprili 2025. 

Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi.

Balile amekuwa Mwenyekiti wa Jukwaa hilo kwa miaka minne baada ya kushinda kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka 2021. Endapo atashinda atakuwa amemaliza kipindi chake cha pili. 

Jumla ya wagombea 14 tayari wamechukua fomu za kugombea ambapo katika nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TEF wamechukua wagombea 12, nafasi ya Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti zina mgombea mmoja mmoja ambako Makamu anayemaliza muda wake Bakari Machumu tayari ameshachukua fomu. 

Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Jumatatu tarehe 24 Machi 2025.


 

0/Post a Comment/Comments