Na Ester Maile _Dodoma
Serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote imejipanga kufikisha huduma za mawasiliano kwa wananchi katika maeneo ya mjini na vijini kwa kujenga minara 758.
Ameeleza hayo Mhandisi Peter Mwaslyanda wakati akizungumza na waandishi wa habari leo 27 march 2025, alipokuwa akieleza mafanikio ya mfuko huo kwa kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwaslyanda amesema UCSAF imejenga minara mingine 430 hadi kufikia tarehe 24 march 2025 minara hiyo imeanza kutoa huduma kwa wananchi.
Hata hivyo mfuko wa mawasiliano kwa wote umefunga intaneti bila malipo (public free WiFi) katika maeneo saba ambapo ni chuo ha maendeleo ya jamii cha Lugambo Mafinga, viwanja vya Nyerere jijini Dodoma ,soko la Taifa Tabora ,kiembe samaki Unguja ,chuo kikuu cha Dodoma, na soko la buhongwa Mwanza na maeneo ya kumi na saba ya viwanja vya maonesho ya sabasaba ikiwalengo ni kuongeza wigo wa matumizi ya intaneti ambapo serikali imetumiakiasi cha milion 374.
Vilevile UCSAF imetoa vifaa vya Tehama kwa shule ishirini na mbili zenye watoto wenye mahitaji maalum moja ya vifaa hivyo ni nuku nundu.
Post a Comment