UMMY MWALIMU AWAKUMBUKA WAFUNGWA NA WENYE MAHITAJI KWA FUTARI

****

Na: Mwandishi Wetu, Tanga

Mbunge wa Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, ametoa vyakula ili viwe futari kwa wafungwa na wenye mahitaji.

Machi 25, 2025, Mbunge Ummy Mwalimu, aligawa vyakula kwa ajili ya wafungwa wa Gereza Kuu la Tanga (Maweni) ili vitumike kama futari kwa wafungwa walio katika mfungo wa Ramadhani na Kwaresma. Vyakula vilivyotolewa ni pamoja ni Sukari Kilo 75, Mafuta Lita 30, Mchele Kilo 500 na Tambi Kilo 300. Vyakula hivyo vilikabidhiwa kwa Afande ACP. Andrew Ntamamiro wa gereza hilo.

Sambamba na hilo, Machi 27, 2025, Ummy Mwalimu aligawa vyakula kwa watu wapatao 100 wenye uhitaji wakiwemo wazee ili waweze kufurahia mfungo. Vyakula hivi viligawiwa kwa wenye uhitaji wanaotambulika na Taasisi ya Jamiyatul Akhlaaqul Islam (JAI) inayojihusisha na kutoa huduma kwa wagonjwa na yatima huku kila mnufaika akipokea kapu lenye vyakula kwa ajili ya kupika futari nyumbani wake.

Katika zoezi hilo, Ummy Mwalimu alisisitiza kuwa ni agizo la Mwenyezi Mungu kuwasaidia watu wenye shida na mahitaji mbalimbali, hivyo ameamua kutoa futari hizo ili watu hao waweze kufurahia na wajione nao ni watu wanaothaminiwa na jamii. Katika hatua nyingine, wanufaika wa futari hizo wamemshukuru Ummy Mwalimu kwa kujitoa kwake na kumuombea kheri katika maisha yake.











 

0/Post a Comment/Comments