******
Na Ester maile _ Dodoma
IKIWA ni mkakati madhubuti wa serikali kukabiliana na wimbi la baadhi ya vijana kukosa ujuzi wa kujiajili na kutegemea serikali pekee,zaidi ya vijana 295175 wamedahiliwa katika vyuo vya ufundi (VETA) katika kozi za muda mrefu na muda mfupi.
Hatua hiyo imetokana na serikali kuongeza vyuo vya VETA nchini kutoka vyuo 41 mwaka 2020 hadi kufika vyuo 80 mwaka 2025.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mkuu wa VETA nchini, CPA Antony Kasore, wakatika akizungumza na waandishi wa habari leo, March 3, 2025 jijini dodoma ikiwa ni miaka minne ya uongozi wa rais Samia Suluhu Hassan.
Ongezeko hili la takriban asilimia 100 ya vyuo vya ufundi stadi nchini linalenga kuiwezeaha VETA kushiriki kikamilifu katika kufikia malengo ya mpango wa tatu wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2025/26 .
Aidha hadi kufikia Juni 2026 vyuo vipatavyo 65 vinatengemewa kukamilika na kuanza kutoa mafunzo hatua itakayo sababisha kuwa na jumla ya vyuo 145 nchini.
Post a Comment