VIBALI 158,820 VYA TOLEWA NA MKEMIA MKUU WA SERIKALI


****

Na Ester Maile _Dodoma 

Mamlaka ya maabara na mkemia mkuu wa serikali imeweza kudhibiti uingizaji na usafirishaji wa kemikali hatarishi na zinazodhibitiwa chini ya mikataba ya kimataifa ilikulinda afya ya binadamu , mazingira na usalama wa nchi kwa kutoa vibali vya kuingiza na kusafitisha kenikali.

Ameeleza haya mkemia mkuu wa serikali Dkt Fidelis Mafumiko leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya mamlaka hyo kwa kipindi vha miaka minne ya Samia suluhu Hassan.

Dkt Mafumiko amesema kwa kipindi cha miaka minne ya serkali ya awamu ya sita kumekuwa na ongezeko la vibali vya uingizaji wa kemikali kutoka vibali 40,270 mwaka wa fedha 2020_2021 hadi kufikia vibali 158,820 desemba 2024 sawa na asilimia 294 ya vibali vilivyotolewa.

Hata hivyo mamlaka imefanya ukaguzi wa maghala katika kuhakikisha kuwa kemikali zinatumika kwa usalama na kwa kufuata taratibu zote zinazohitajika.

Mwisho mamlaka inatarajia kupata hati safi kwa vitabu vya mahesabu vya mwaka wa fedha 2023_2024 ambapo ripoti itatolewa mwaka wa fedha 2024_2025.



 

0/Post a Comment/Comments