******
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanikiwa kupunguza udanganyifu ambapo mfuko umeokoa zaidi ya Bilioni 22 kwa kufanya chunguzi 259 kwenye vituo vya afya .
Akibainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Mfuko huo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 10, 2025 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dkt. Irene Isaka amesema kuwa zaidi ya kadi 13,000 za wanachama zimefungiwa hususani wanachama waliokuwa wakitumia kadi moja kwa zaidi ya mtu mmoja.
Ameongeza kuwa watumishi 36 wa vituo vya afya wameripotiwa kwenye bodi zao ambao wamehusika na udanganyifu na NHIF wamechukua hatua kwa watumishi ambao wameonekana wamehusika kwenye udanganyifu wamechukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma.
Aidha amesema kuwa vituo 11 vimefungiwa kutokana na udanganyifu na hatua hiyo inafanyika kwa umakini mkubwa kwani serikali inaongeza juhudi kuongeza vituo vya afya.
Post a Comment