Akizungumza leo Machi
27, 2025 katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Bodi, Waziri Kikwete ameelekeza Bodi
hiyo kusimamia Sera, Sheria, Kanuni, kuzingatia miongozo mbalimbali inayotolewa
na Serikali pamoja na kusimamia misingi ya uwajibikaji, uadilifu, ubunifu na
ushirikiano katika kazi.
"Misingi hii ni muhimu kwa sababu inahakikisha PSSSF
inafanya kazi kwa ufanisi, usawa na haki, kuepuka rushwa kwa watumishi na
viongozi katika kuhakikisha Mfuko unakua endelevu na kukuza uhimilivu
wake," alisema Mhe. Kikwete.
Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bi. Mary Mapunjo ameshukuru
kwa uteuzi wa wajumbe wa Bodi ambapo amesema kuwa uteuzi huo umezingatia
taaluma mbalimbali ambazo zitawezesha ustawi wa Mfuko na kuupongeza utendaji
kazi wa PSSSF.
"Wajumbe wa Bodi hii uteuzi wake umezingatia taaluma
zote muhimu, kumekua na mchanganyiko mzuri tunaamini kazi itatendwa
vizuri," alisema Bi. Mapunjo.
Aidha amesema kuwa Bodi mpya imepokea maelekezo yote
aliyotoa na kuahidi kuwa wamejiwekea mikakati ya kutenda kazi kwa kasi ya
kukimbia kuendelea pale ambapo Bodi iliyopita ilipoishia.
Post a Comment