Taarifa ya Yanga iliyotoka usiku huu kufuatia kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo iliyokutana kwa dharura imesema haitarudiana na watani wao hao kufuatia mchezo huo kuzuiwa Machi 8, 2025 na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB).
Kwenye taarifa hiyo Yanga imetoa maazimio matatu ya Kamati yao ya utendaji ikisema inataka kupewa ushindi kwa mujibu wa kanuni pindi timu moja inaposhindwa kutokea uwanjani.
Yanga pia imelitaka Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ kuvunja Kamati ya usimamizi wa ligi iliyo chini ya Mwenyekiti wake Steven Mnguto (Mwenyekiti wa TPLB) na katibu wake Almas Kasongo (Afisa Mtendaji Mkuu TPLB) kwa kile ilichoeleza kukosa imani na Kamati hiyo na kuweka watu wenye nia njema na yenye waadilifu kwa maslahi ya mpira.
Aidha imesema haitakubali kurudiana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara namba 184.
Post a Comment