ANAYEDAIWA KUMJERUHI PADRI KITIMA AKAMATWA


               ::::::

 Jeshi la Polisi lina mshikilia mtu.mmoja kwa tuhuma za kumjeruhi Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Padri Charles Kitima.

Padri Kitima anadaiwa kujeruhiwa na watu wawili akitoka maliwatoni muda mfupi baada ya kumaliza kikao na viongozi wa dini. 

Taarifa ya Jeshi la Polisu kwa vyombo vya habati imesema kuwa watu hao wanadaiwa kumjeruhi Padri Kitima baada ya kumpiga kichwani na kitu butu. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya tukio hilo, Padri Kitima alipelekwa katika Hospitali ya Agha Khan kwa matibabu na sasa anaendelea vizuri.

0/Post a Comment/Comments