****
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa, amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, katika mazungumzo yaliyolenga maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yanayofanyika mkoani humo.
Balozi Mussa amepongeza maandalizi ya mkoa huo na kusifu mchango wa michezo katika kuimarisha afya na mshikamano kwa watumishi wa umma. Ameeleza kufurahishwa na mafanikio ya Timu ya NJE Sports, iliyofuzu hatua ya robo fainali katika michezo ya netiboli na soka.
Amesema ushiriki wa Wizara hiyo kwenye michezo unaonyesha kuwa diplomasia haijafungwa tu katika uwanja wa kimataifa, bali pia inajumuisha ustawi wa watumishi katika shughuli za ndani.
Kwa upande wake, Mhe. Dendego amemshukuru Balozi Mussa kwa ujio wake ambao umewapa hamasa na kutambua mchango wa NJE Sports kwenye shamrashamra hizo.
Balozi Mussa aliambatana na Mwenyekiti wa NJE Sports, Bw. Ismail Abdallah, na Kocha Shaban Maganga.
Post a Comment