CCM : MUUNGANO WA TANZANIA UTALINDWA KWA NGUVU ZOTE


 *******

Na Mwandishi Maalum , Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Amani, Usalama na Utulivu wa Tanzania kwa miaka  61 , umetokana na misuli ya Ulinzi chini ya  Serikali ya Jamhuri  ya Muungano  Tanzania .

Pia kimewataka Wananchi  kupuuza maadai ya   upinzani  yanayoelezwa kuwa Zanzibar itakawia kupata maendeleo   kwa kukosa  Mamlaka kamili.

Matamshi  hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Zanzibar ,  Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ,Khamisi Mbeto Khamis ,alipozungumza na   Waandishi  wa habari  katika Afisi Kuu ya CCM  Ksiwandui .

Mbeto alisema Usalama na Utulivu  wa pande mbili  za Muungano   tokea Mwaka 1961 kwa  upande wa Tanganyika na Zanzibar kuanzia   Mwaka 1964,  baada ya hapo Muungano  ndio  unaosimamia maendeleo  na  Usalama wa Taifa . 

Alisema nje ya  Muugano wa Tanzania, si Tanganyika wala Zanzibar ambazo zingeweza kuhimili  harubu na misukosuko ya kusimamia  Ulinzi na Usalama bila  Muungano . 

Alisema wanaoshabikia na kutaka Muungano  uvunjike aidha watakuwa na   ajenda za siri  au ni  vibaraka wanaotumiwa na maadui dhidi  ya  ustawi  wa Umoja na Maendeleo.

Amewataka wanaotamka maneno hayo ni  wazi watakuwa wameleweshwa na  hali ya  Utulivu na Amani   iliopo kwa miaka mingi  huku wakijua  wanalindwa na  serikali  ya Tanzania. 

"Usalama wa Zanzibar na Tanganyika ni kutokana na  Muungano . Nje ya Muungano hakuna Tanganyika wala Zanzibar .Utachomoza ukabila na ubaguzi. Huyu Mpemba ,yule Muunguja , hawa wamehamia toka Oman na   Bara na wale kule ni Wangazija na Wahindi    " Alisema Mbeto 

Aidha Mwenezi   huyo  akitoa mfano ,aliutaja Muungano wa Nchi mbili za  Tanzania  si jambo geni  duniani  kwani kuna Muungano  Umoja  wa Nchi  za  Falme za Kiarabu  wenye nchi  nane  chini ya UAE.

Akizitaja nchi hizo  alisema  ni Dubai Abuudhabi, Sharja na  Ras al Hema  .

Nyingine ni Ajman, Amulhuwein, Fujera na Olfaghan .

"Maendeleo ya UAE  yametokana na Muungano. Nchi nane zina Dola moja ya  UAE  .UAE ni mfano wa Maendeleleo ya Muungano   duniani. Wanaoota Muungano wa Tanzania utavunjike watasubiri kwa miaka mingi  "Alieleza 

Alisema,Zanzibar  imepata  maendeleo ya ghafla  baada ya Ufalme  kudondoka kwa  miaka minane chini ya  Rais  Abeid Amani  Karume , baada ua hapo tukaungana na wenzetu  Tanganyika ,hadi sasa sasa tunaishangaza dunia 

"Leo Zanzibar  inatazamwa kivingine   kwa maendeleo   yaliotokea kwa miaka mitano ya Rais  Dk Hussein  Mwinyi  , baada ya miaka kumi  Zanzibar itakuwa  kama Dubai ,Hong Kong  au Singapore " Alieleza Mbeto.

0/Post a Comment/Comments