Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelitaka Jeshi la Magereza, mamlaka husika pamoja na vyombo vya dola kutoa taarifa za haraka kuhusu mahali alikopelekwa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.
CHADEMA imetoa taarifa hiyo baada ya kudai kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Wakili Ali Juma, mawakili, familia pamoja wanachama walifika katika gereza la Keko ambapo Lissu anashikiliwa, na kuambiwa kuwa hayupo bila maelezo yoyote.
Post a Comment