Na Aziza Masoud,Dar es Salaam
JAMII imetakiwa kubadilika na kuacha kutumia njia za kizamani zakualika watu katika matukio mbalimbali badala yake watumie njia zakidigitali ili kuokoa muda na kupunguza usumbufu.
Akizungumza jana Meneja wa Mawasiliano wa Envaita Praygod Mushi alisema utumiaji wa mialiko ya kadi kwa njia ya kidigitali unaokoa mambo mengi japokuwa watu hawana imani nazo.
"Njia ya kidigitali ni nzuri lakini changamoto iliyopo watu bado hawaelewi wanadhani ni utapeli,pia kumekuwa na mtazamo mtu akitumiwa kadi za mialiko kwa njia ya simu anaona amedharaulika, lakini ndiyo njia sahihi na inayofaa katika kipindi hiki cha utandawazi wakidigitali,"alisema Mushi.
Alisema mialiko ya kidigitali pia inasaidia kupanga bajeti kwakuwa unakuwa na idadi kamili ya watu wanaohudhulia tukio lako.
Akizungumzia kuhusu kampuni ya Envaita imekuwa ikitoa huduma za kutoa mialiko kidigitali alisema huduma hiyo ni gharama nafuu na rahisi kufikika.
"Mialiko yakidigitali yote inatumwa kwa njia ya Whatsapp uwe na smart ama huna unapata mwaliko wako,Kwa wale wasiokuwa na simuza smart wanatumiwa kwenye simu ndogo namba zao za kadi na taarifa zao zote zinakuwa mtandaoni.
"Pia kuna watu unaweza ukamtumia mwaliko labda asielewe na akahisi kuwa ni utapeli sisi uwa tunapiga simu kuwapa taarifa ili wasiwe na wasiwasi,siku ya sherehe pia tunahudhulia kwa ajili ya kuscan kadi,"alisema Mushi.
Alisema kadi haiwezi kutumika mara mbili Wala hakuna atayeweza kuingia kwenye sherehe bila kualikwa.
Alisema baada ya shughuli kampuni inatuma ujumbe mfupi wakuwashukuru watu ambao inatoka kwenye familia.

Mwisho
Post a Comment