******
Wananchi wa halmashauri ya Chalinze mkaoni Pwani wamefikiwa na skimu ya hifadhi ya Jamii inayoendeshwa kwa Jina la ‘’STAR WA MCHEZO’’ na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF kwa nchi nzima lengo ikiwa ni kuwafikia wajasiriamali wote wadogo wa hapa nchini ili waweze kupewa elimu ya hifadhi ya jamii kwa Manufaa yao ya sasa na ya baadae.
Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika Tarehe 30.03.2025 katika soko la Bwilingu lililopo katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze na Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, kazi, Vijana na wenye ulemavu, Ridhiwani Kikwete ambaye amepongeza mwitikio mkubwa wa wananchi walijitokeza katika uzinduzi huo na kujiandikisha huku akieleza umuhimu wa kuweka akiba kupitia skimu hiyo ya hifadhi ya Jamii.
Awali kabla ya kuzungumza mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF Omary Mziya ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi mkuu wa NSSF amemshukuru Mhe waziri kwa kufanya uzinduzi huo na kubainisha makundi yatakayonufaika na hifadhi hiyo ya skimu kuwa ni kwa Vijana, akina mama na akina baba waliojiajiri katika Maeneo ya kiuchumi.
Kwa upande wake Rehema chuma Meneja Nssf anaeshughulikia Wananchi Waliojiajiri katika uzinduzi huo amepata nafasi ya kuelezea Kampeni hiyo ya Star wa Mchezo huku akisema lengo la Serikali ni kuhakikisha watanzania wanakuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba ili waweze kuwa na uzee wenye staha.
Nae Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga amefuhishwa na ujio wa NSSF na Skimu ya hifadhi ya jamii katika halmashauri hiyo kwa kuwa anatambua umuhimu wake, amewahakikishia wananchi waa chalinze na bagamoyo kuwa skimu hiyo ni mkombozi wa maisha ya baadae na amewahakikishia NSSF kuipokea Skimu hiyo na watarajie utekelezaji mzuri katika skimu hiyo.
Nao baadhi ya wafanyabiashara wadogo wa Soko la Bwilingu walioshiriki uzinduzi kwa kampeni hiyo akiwemo Vicenti Magoti wao wamejiajiri, baada ya kupata elimu wamejiunga kuwa wanachama, wameishukuru NSSF kwa kufikisha kampeni hiyo kwao ambapo wanatarajia kupata manufaa makubwa kwa maisha ya Sasa na ya baadae.
Kupitia kampeni ya STAR WA MCHEZO endapo mwanachi atakuwa mwanachama atanufaika na mafao Mbalimbali yakiwemo Mafao ya Pesheni ya uzee, Mafao ya urithi , Mafao ya ulemavu,mafao ya uzazi na Matibabu na walengwa wa skimu hiyo ni wafugaji, wavuvi, wakulima, machinga, bodaboda na wachimbaji wadogo wa Madini.
MWISHO
Post a Comment