Na Ester Maile Dodoma
Maafisa Habari wa Serikali
watakiwa kutambua ujio wa Kikao Kazi ni kwa ajili ya kufundwa na kuzingatia yote yatakayoelekezwa na kukumbushwa juu ya utekelezaji wa majukumu yao.
ameyanabaisha hayo katibu wa habari,utamaduni, sanaa na michezo Gerson Msigwa wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha 20 cha Maafisa Habari wa Serikali kinachofanyika katika Hoteli ya New Amaan Zanzibar, leo Aprili 3, 2025.
Aidha, Msigwa ametaja malengo ya Kikao Kazi hicho kwa Maafisa Habari wa Serikali kuwa ni kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma kupitia programu za kujenga uwezo kwa watumishi pia kuimarisha Muungano na kubadilishana uzoefu.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Tabia Maulid Mwita, ameshukuru kukubaliwa ombi lake la Kikao Kazi hicho kufanyika Zanzibar na kutaja sababu kuu ya kufanya hivyo ikiwemo Maafisa Habari kujionea shughuli mbalimbali za utalii, michezo na maendeleo makubwa ndani ya Zanzibar.
Tabia amesema Lengo kubwa la kuomba Kikao Kazi hicho kufanyika Zanzibar ni kuendelea kuimarisha Muungano wetu, pili ni kuwawezesha Maafisa Habari kuja kuiona Zanzibar ya sasa ya Dkt. Hussein Ali Mwinyi, hivyo watapata kibali cha kuisemea Zanzibar kule Tanzania Bara na duniani
Vile vile ameahidi kwamba, Wizara yake ya Habari Tanzania Zanzibar itaendelea kushirikiana na Wizara ya Habari Tanzania Bara katika nyanja zote zinazohusu sekta ya Habari nchini.
Wakati mafundo hayo yakiendelea, kikao hicho kimetoa fursa ya upimaji wa afya bure kwa wadau wote wa habari wanaoshiriki kikao hicho na wananchi watakaofika katika viwanja vya Hoteli ya New Amaan ambapo madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, MOI, JKCI na Lumumba wanaendelea kutoa huduma za afya za kibingwa kuanzia leo Aprili 3, 2025 hadi ukomo wa kikao hicho Aprili 6,2025.
Post a Comment