*****
Na Mwansishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimemuonya Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ,Ismail Jussa Ladhu na kumtaka aache tabia za uongo na kudai kuna wana CCM zanzibar wanaounga mkono upinzani.
CCM kimesikitishwa na matamshi hayo na kuyaita ni maneno ya mfamaji anayetapatapa ili kujinusuru asizidi kuzama chini ya kina kirefu cha bahari .
Hayo yameelezwa na Katibu Kamati Maalum ya Nec Zanzibar, Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo ,Mbeto Khamis Mbeto, aliyemtaka Jussa kufuta ndoto zake kama CCM kitashindwa uchaguzi oktoba mwaka huu.
Mbeto alisema kadri Jussa anavyojitahidi kutaka kumbagua Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi, hawezi kusikilizwa na watu waungwana kwakuwa amezaliwa zanzibar , kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini unguja kama yeye alivyozaliwa Makunduchi Mkoa wa Kusini .
Alisema Jussa hana ubavu,mbinu wala jeuri ya kumbagua Rais Dk Mwinyi kwa asili yake, rangi au kwa nasaba yake , kabla ya jamii ya kizanzibari hawajambagua Jussa kwanza kutokana na historia na chimbuko la asili na nasabu yake.
"Jussa acha kuwaghilibu wananchi wa Zanzibar kwa kujipa chati ya uzanzibari .Babu na bibi yake wamekuja Zanzibar kufanya kazi ya kupeta mpunga na kuuza vyungu katika mitaa Mapipa ya Ngozi, Mchangani na Vikokotoni" Alisema Mbeto.
Pia Katibu huyo Mwenezi aliwataka wazanzibari kuendelea kumpuuza kijana huyo kila anapopanda majukwani na kuropoka kwani amekubuhu katika Siasa za uzushi , ugombanishi na kubuni mifarakano.
"Wewe Jussa cha kuwataja wanasiasa waliofukuzwa CCM mwaka 1987 ili kujionyesha kama anawajua kuliko watu wengine.Jussa ni bwana mdogo na mshamba anayependa kujikweza .Ni mpayukaji aliyegikwa taji la ufedhuli na ukosefu wa adabu" Alieleza
Aidha , Mbeto alisema hatua ya Makamu huyo Mwenyekiti kutaja majina ya wanachama saba waliofukuzwa CCM mwaka 1987 wakiwa na Maalim Seif Sharif Hamad ,waliondoshwa ili kujenga umoja ndani ya Chama .
"Jusaa amejaaliwa uso uliokosa aibu .Anasimama na kudai Maalim Seif alikuwa akimheshimu sana Hayati Sheikh Idrisa Abdul wakil wakati ndiye aliiyesibabisha hadi Rais huyo akajiuzulu urais kabla ya muda wake "Alieleza Mbeto
Aliongeza kusema Jussa kwa hulka na tabia yake ya kujipendekeza,alifanikiwa kumgombanisha Maalim Seif na wanasiasa wenzake kina Hamad Rashid Mohamed ,Mussa Haji Kombo ,Khatib Hasan Khatib na Mohamed Dedes.
"Wakati Rais Mstaafu Dk Amani Karume akiwa madarakani Jussa ndiye aliyekuwa akiongoza kumdhihaki na kumwita ni raia wa Malawi. Leo kwa tabia yake ya kigeugeu anamsifu kinafiki akidhani atamuunga mkono "Alisisitiza Mbeto
Katibu huyo Mwenezi aliongeza kusema Jussa ndiye aliyekuwa akimpachika majina ya kejeli Dk Karume akimwita 'hapa pangu',' Chaijaba na "Ahmada hiyo akijaribu kumvunjia heshima yake kiongozi huyo mstaafu .
Post a Comment