*****
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Chama cha Mapinduzi (CCM ) kimewataka makada wake, viongozi na wanachama kutetea sera za chama , kuwalinda na kuzungumzia mafanikio ya kazi zilizofanywa na marais wawili, Rais Dk Samia Suluhu Hassan na Rais Dk Hussein Ali Mwinyi.
Pia wanachama wa chama hicho wamekumbushwa wajibu wa kuhubiri maendeleo yaliofanyika kwa muda mfupi chini ya maraisi hao wawili.
Ushauri huo umetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis , alipokuwa akizumgumza na wanachama wa Taaisis inayojihusisha na Utetezi kwa Mama katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui .
Mbeto alisema majukumu ya kumtetea Mama , Rais Dk Samia yaendelee , yafanyike kwa kasi ya kutosha , usahihi na ufasaha, kwa kuonyesha vielelezo, data na takwimu kwa kazi zilizotekelezwa na serikali zao tokea waliposhika madaraka.
Alisema vipimo vya utendaji na utekelezaji wa sera ,ilani ya uchaguzi ya CCM ,miradi ya maendeleo katika sekta zote, Rais Dk Samia na mwenzake Rais Dk Mwinyi wametia fora.
" Timizeni wajibu wenu mkiwa Wakereketwa , makada wa chama, viongozi na wanachama wa CCM. Nyinyi wana CCM mkinyamaza wapinzani watapotosha.Njia pekee bora ni kusimama na kuelezea yote yaliofanyika"Alisema Mbeto.
Aidha Katibu huyo Mwenezi, aliishauri Taasisi hiyo kutofanya kazi hiyo kwa kupiga maneno matupu, badala yake ikusanye data, takwimu na vielelezo vitakavyoonyesha utendaji kazi kwa vitendo.
"Binadamu tuna kawaida na hulka ya kuona vitu na kusahau haraka. Hivyo ni wajibu wenu kuendelea kutangaza kazi zilizotekelezwa kisekta. Fanyeni kazi hii bila kuchoka kwakuwa siasa ni kazi ya kujitolea kufa na kupona "Alieleza.
Alisema marais Dk Samia na mwenzake Rais Dk Mwinyi uongozi wao, utaacha alama nyingi za kimaendeleo ambazo hazitafutika na kusahaulika miaka kwa miaka .
"Hata wapinzani wetu wakiwa peke yao wanakiri kazi kubwa imefanyika. Tanzania na Zanzibar ya jana na juzi sio ya leo. Hawataki kutamka hivyo hadharani wakiamini vyama vyao vitakufa" Alisiaitiza Mbeto
Kadhalika aliongeza kusema maendeleo yanaonekana waziwazi katika sekta zote muhimu za Afya, Elimu, Ujenzi wa Miundombinu , Maji , Kilimo, Ufugaji ,Uvuvi, Nishati ,Utalii na uwekezaji .
Post a Comment