RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MKURUGENZI MTENDAJI TANESCO

 

......,.......

Kupitia ukurasa wake wa mtandao kijamii Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameandika "Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya Mhandisi Boniface Gissima Nyamohanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), pamoja na dereva wake, Muhajiri Mohammed Haule, vilivyotokea usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya barabarani eneo la Bunda, Mkoa wa Mara.

Ninatoa pole kwa familia, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko, watumishi wa TANESCO, ndugu jamaa na marafiki.

Namuomba Mwenyezi Mungu azijaalie familia, ndugu, jamaa na marafiki subra, uvumilivu na moyo wa ibada katika kipindi hiki kigumu.

Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi.

Amina.

Vilevile kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mkurugenzi ya Mawasiliano ya RAIS Ikulu Rais Dkt Samia ametumia salamu za rambirambi kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko

0/Post a Comment/Comments