RAIS SAMIA YUPO KAZINI - MKURUGENZI MIGERA


 *****

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kina masikio mapana ya kumsikiliza Mwananchi wa hali yoyote bila kubagua daraja la Elimu aliyonayo.

 Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Jamii Kwanza initiative (JKI) na Kada ya chama hicho, Daniel Migera amesema Chama hicho kimeweka misingi mikubwa sana kwenye ilani yake hasa ya Elimu bure na stahiki kwa wakati.

"Katika ilani ya Chama chetu suala la Elimu bure ni jambo zuri ambalo serikali imelipa kipaumbele, Na tunaona kwasasa watoto hawapati shida wala kurudishwa mashuleni bila ada hivyo jambo hili la Elimu bure ni jambo zuri, " amesema Migera.

 Akizungumzia Mikutano ya Kimataifa kufanyika nchini Tanzania Migera alisema hii inadhihirisha Rais Samia na Chama cha Mapinduzi kinaaminika kwasababu kila anachoahidi anatekeleza na ni mtu wa vitendo na miradi yote anaitekeleza.

 "Matokeo na Maendeleo yanayooneka ni Juhudi na Uchapakazi wa Rais samia ambaye amejikita kutatua changamoto za Watanzania.

Kuhusu utekelezaji wa Miradi amepongeza miradi iliyofanywa na Rais samia kama vile Treni ya Mwendokasi (SGR), Mradi wa kufua umeme wa JNHPP na Ujenzi wa Daraja la Busisi.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi Migera amesema kuwa ziara za nje ya za Rais Samia zimeleta mafanikio makubwa,kwa sababu anatoka kwenda kutafuta.

"Wanaochukia ziara za Rais Samia wajitafakari na wajiulize kama Huwa wanakaa nyumbani na chakula kinakuja chenyewe au unaenda Kutafuta? Mimi kama kada wa CCM nasema mama yuko kazini"Amesema Migera

0/Post a Comment/Comments