********
Na Mwandishi Wetu.
Taasisi ya Demokrasia na Maendeleo Tanzania (TADED) imesema kuwa hakuna chama au taasisi ya kufanya kuzuia uchaguazi Mkuu ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa TADED Chalila Kibuda amesema kuwa kwa mujubu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga kura ni haki ya watanzania hivyo hawezi chama au Taasisi kuwazuia wananchi wasipige kura.
Amesema TADED katika kipindi cha kuelekea uchaguzi kitahakikisha kinahamasisha wananchi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi mkuu katika kusikiliza mikutano ya kampeni kutoka kwa wagombea pamoja na kushiriki kupiga kura.
Amesema katika kampeni hizo kwa wagombea kunadi sera za vyama vyao na sio kukashifiana ambapo hizo kashfa sio kipaumbele kwa wananchi wanaotaka maendeleo kwa viongozi wataowachagua.
"Uchaguzi huu ni haki ya kila mwananchi kushiriki katika kuchagua viongozi wataodumu kwa kipindi cha miaka mitano kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania".amesema
Aidha amesema suala la chaguzi Mkuu kwa katiba hii hakuna chombo chochote kinachoweza kuzuia kutofanyika uchaguzi ambapo hata chama kilichopo madarakani hakiwezi kufanya hivyo.
Hata hivyo katika maandalizi hayo yamefanyika vizuri ikiwemo wananchi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura nchi nzima.
Kibuda amesema chama fulani kinasema No Reform.No election ni
jambo ambalo haiwezekani kuleta katikati ya zoezi hilo kuanza.
Hata hivyo tangu tumefanya uchaguzi 2020 katika
kipindi hicho walikuwa nafasi ya kufanya juu ya kuliendea jambo la uchaguzi na
serikali ikachukua hatua.
Hata hivyo Serikali ya awamu ya sita chini Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuweka utulivu wa Siasa amefanya mambo pamoja na kuwa na maridhiano ya kuruhusu mikutano kufanyika ambapo vyama vinaendelea kufanya mikutano bila vikwazo.
Aidha katika mazingira tulionayo nchi iko tulivu
kabisa kila mwananchi anaendelea kufanya maisha yake hii inaonyeesha amani
ambapo Rais na vyombo vyake kuendelea
kuhudimia wananchi wake.
Katika mikakati iliyojiwekekea Taasisi ni
pamoja na kufanya makongamano nchi nzima
kwa kushirisha wasanii mbalimbali ambapo mazungumzo yao yanaendelea kufanyika
na hatuwezi kuyatoa kwenye vyombo vya habari pamoja na kukutana viongozi wa wa
dini katika katika kilele cha kampeni viongozi hao kutoa ujumbe kuhusiana na
uchaguzi.
Post a Comment