TCB YAZINDUA KAMPENI YA "TOBOA KIDIJITALI " KUHAMASISHA UJUMUISHI WA KIFEDHA


 *****

Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imezindua kampeni mpya ya kitaifa iitwayo “Toboa Kidijitali,” yenye lengo la kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kisasa ya miamala ya kifedha na kuongeza ujumuishi wa kifedha nchini.

Akizungumza  wakati wa uzinduzi huo Uzinduzi wa  kampeni hiyo leo jijini Dar  es salaam  kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Adam Mihayo, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi na Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati, Bi. Lilian Mtali, amesema benki imewekeza zaidi ya shilingi milioni 200 katika kampeni hii kama sehemu ya kurudisha kwa jamii, na pia kukuza matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya kidijiti,huku akisisitiza kuwa TCB inaendelea kuboresha huduma kama Popote Mobile App, Popote Visa Card na mfumo wa Lipa Popote, ili kuwawezesha wateja kufanya miamala bila usumbufu na kwa usalama.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Huduma za Kidijiti na Ubunifu wa TCB, Jesse Jackson, amesema kampeni ya Toboa Kidijitali inatoa fursa kwa wateja kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo gari aina ya Mazda, simu ya iPhone 16 Pro Max, pamoja na bodaboda na bajaji kila mwezi kwa kipindi cha miezi minne, lengo ni kuchochea matumizi ya mifumo ya kifedha ya kidijiti na kuvutia makundi mbalimbali ya Watanzania, hasa walioko vijijini na maeneo ya pembezoni.

Jackson ameongeza kuwa ingawa kuna ongezeko la miamala ya kidijitali kutoka milioni 14 mwaka 2020 hadi milioni 21 mwaka 2024, bado Watanzania wengi hutegemea fedha taslimu, hivyo, TCB imeona umuhimu wa kutoa elimu na motisha kwa umma kupitia kampeni hii, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha ujumuishi wa kifedha na kupunguza utegemezi wa cash economy.













0/Post a Comment/Comments