TMDA YATOA KOMPUTAR CHUO KIKUU KAMPALA


*****

Na Tausi Mbowe

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), imetoa msaada wa komputa mpakato mbili kwa Chuo Kikuu cha Kampala tawi la Tanzania. 

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jumatatu Machi 7, 2025 jijini chuoni hapo Gongolamboto jijini Dar es Salaam. 

Akikabidhi kompyuta hizo mpakato, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Gaudensia Simwanza alisema msaada wa Mamlaka hiyo ni sehemu ya uwajibikaji wa taasisi jamii. 

"Lengo ni kusaidia jamii na kuwezesha wanafunzi taasisi inawajibu wa kurudisha kwa jamii, " alisisitiza Simwanza. 

Kwa mujibu wa Simwanza, pamoja na kusimamia masuala ya afya kwa Watanzania pia inapaswa kurudisha kwa jamii. 

Mamalaka ya Dawa na Vifaa tiba Tanzania (TMDA) ni taasisi inayosimamia  masuala  yote yanayohusu dawa vifaa tiba na vitendanishi..


0/Post a Comment/Comments