USHIRIKIANO WA TCB NA RAMANI KUIMARISHA BIASHARA ZA NDANI


****

Benki ya Biashara Tanzania (TCB) kwa kushirikiana na Ramani.io wamezindua rasmi ushirikiano unaolenga kuimarisha biashara za ndani na kuongeza ujumuishaji wa kifedha nchini wakilenga kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya biashara, ikiwemo kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs), wajasiriamali, pamoja na biashara ndogondogo.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa kutia hati ya Makubaliano (MoU) inayoweka msingi wa ushirikiano huu wa kimkakati, Jesse Jackson, Afisa Mkuu wa Digitali na Ubunifu TCB amesema Benki ya Biashara Tanzania inaamini katika kujenga ushirikiano ,hivyo Ushirikiano huo na Ramani.io utatusaidia kuwafikia wafanyabiashara wengi Zaidi kwa urahisi na haraka na pia kuwasaidia kukua kwa pamoja na kujenga uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Iain Usiri Mkurugenzi Mtendaji (CEO) na Mwanzilishi Mwenza wa Ramani, amesema kuwa Ushirikiano huu kati ya TCB na Ramani io unaweka kiwango kipya cha ubunifu na ushirikiano katika sekta ya kifedha, ukiwa mfano wa kuigwa wa namna ya kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha na kukuza biashara za ndani lakinibpia ni uthibitisho wa wazi wa dhamira ya pamoja ya kuendeleza uchumi jumuishi na endelevu nchini Tanzania.

Kupitia ushirikiano huu, changamoto katika mnyororo wa ugavi na usambazaji zitashughulikiwa kwa kutumia teknolojia bunifu ya Ramani.io sambamba na huduma bora za kifedha kutoka TCB yenye mtandao mpana kuongeza,Lengo ni kuwawezesha wafanyabiashara kupata mitaji kwa urahisi, kuongeza ufanisi wa uendeshaji, na kukuza biashara zao kwa njia endelevu.


0/Post a Comment/Comments