BALOZI.DKT. MWAMPOGWA ASIPOGOMBEA UBUNGE UCHAGUZI MKUU WA 2025 ATAWAKATISHA TAMAA WATOTO WA MASIKINI VIJIJINI

.......

Na: Mwandishi Maalum.

Je, unamfahamu Balozi.Dkt. Mohamed Mwampogwa wewe? Kama ndiyo, jambo jema, kama humfahamu, basi fuatana nami katika makala hii fupi kumuhusu kijana huyu mzalendo wa Tanzania.

Balozi. Dkt. Mwampogwa ni Mwalimu kwa taaluma, Afisa Sanaa na Utamaduni, Askari wa Jeshi la Akiba nchini, Afisa Mawasiliano ya Umma, Kijana kutoka familia ya kimaskini ya kijijini kabisa.

Yapo mambo ya kipekee kabisa kumuhusu kijana huyu; Fuatana nami, usichoke. Balozi Dkt. Mwampogwa ana Shahada nne (4) za Udaktari wa Falsafa wa Heshima katika Uongozi Mipango na Usimamizi, Maendeleo ya Jamii, Utumishi wa Umma na Mawasiliano ya Umma. Vilevile, nii Balozi wa Amani Duniani anayetambuliwa na Shirikisho la Amani Duniani (UPF). Kwa hakika kijana huyu ni alama ya uzalendo na  nembo ya watoto wa masikini hasa waliopo vijijini.

Balozi.Dkt. Mwampogwa ni muasisi wa falsafa ya uzalendo huru na kujitolea nchini ambaye kaisimamia falsafa hii kwa miaka 11 na jina lake linavuma mno mithili ya kimbunga katika kila wilaya nchini Tanzania. Kijana anapenda kujituma kwa moyo, anapenda taifa, muda wote ana hali ya tabasamu usoni na moyoni.

Kijana huyu anawajibika sana siku zote bila kudai malipo hali ambayo kwa kweli imemfanya kufunguliwa milango na kuwa na marafiki wengi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Aidha, ni kijana mpenda watu, mwenye moyo safi, ubongo uliojaa maarifa mengi ya darasani na ya maisha ya kawaida ya kila siku. Sanjari na hilo, ni mtetezi wa wanyonge, mkweli na muwazi sana na mpenda maendeleo. Ni mwamba haswa na mwenye ushupavu hasa katika ujengaji wa hoja imara zenye kutetea maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kimsingi, wakati tunaelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba 2025, Wazalendo Huru Tanzania wapatao 685,000 (Laki sita na Themanini Elfu) nchini ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huenda wanamtazama mzalendo huyu kuwa atafanyaje. Je, atatia nia  ya kugombea ubunge katika moja ya majimbo nchini?

Balozi.Dkt. Mwampogwa pia ni msanii wa muziki wa asili na kizazi kipya anaendelea kuwa alama ya kutunzaji utamaduni wetu na anabaki kuwa hazina isiyoweza kulinganishwa na kijana yeyote katika makundi ya vijana. Ni nani ambaye hamtazami Balozi Dkt. Mwampogwa kama kijana mzalendo na mwenye ushawishi wa wazi nchini?

Binafsi naamini asipogombea Ubunge tafsiri yake anawazuia kisaikolojia vijana shupavu, wazalendo wa kweli na makada watiifu wa CCM wanaotoka katika Jukwaa la Wazalendo Huru nchi nzima kupoa sana katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

Nimpe hongera za dhati Balozi.Dkt. Mwampogwa kwa kazi uzuri aliyoifanya ndani ya miaka 11 na ikaweza kutuzalishia vijana wazalendo wanaong'ara na walio imara katika sehemu mbalimbali nchini. Orodha ni ndefu, lakini kutaja kwa uchache baadhi yao ni pamoja na: Dk.Calamba (Mkuu wa Shule na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya), Dk.Catherine Mapunda (Afisa Elimu Kata) na Dk.Upendo Sanare.

Wengine, Dk.Hadija Issa (Mdhibiti Ubora wa Shule), Dk.Daudi Msuya, Dk.John Jumanne (Mkurugenzi wa Joboju African Company).Pia wapo Dk.Irene Mashine, Dk.Julieth Anael (Afisa Elimu Kata), Dk.Dismass Lyassa, Dk.David Mramba (Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani), Dk.Vumilia Simbeye (Mkurugenzi Kasulu Mji), Dk.Ahmad Mtenguzi na wengine wengi.

Huyu ndiye Balozi.Dkt. Mwampogwa ambaye natamani nimuone akitia nia ya Ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba, 2025. Ni ukweli kuwa Balozi.Dkt. Mwampogwa anaweza kuwawakilisha na kuwasemea wananchi katika muhimili muhimu wa kutunga sheria yaani Bunge.


 

0/Post a Comment/Comments