CPA SULUO APONGEZA MAONO YA RAIS DKT. SAMIA KUPITIA FALSAFA YA 4R

::::::::

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), CPA Habibu Suluo, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake thabiti unaoongozwa na falsafa ya 4R (Reconciliation, Resilience, Reforms, Rebuilding), akisema kuwa maono hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarika kwa taasisi hiyo.

Akizungumza katika semina ya wanahabari mabalozi wa Mamlaka hiyo leo Mei 6, 2025 Kibaha - Pwani, Suluo amesema kuwa falsafa ya 4R imetoa mwelekeo mpya kwa taasisi nyingi nchini, ikiwemo LATRA, ambapo utekelezaji wake umeimarisha mifumo ya utendaji na kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi.

“Maono ya Rais Samia alivyokuja na 4R yametusaidia LATRA kusonga mbele. Tunampongeza kwa kutuonesha njia sahihi ya utendaji, na sisi tunawajibika kuyafuata maono yake,” amesema Suluo.

Aidha, ametoa pongezi kwa mabalozi wa LATRA kwa kazi yao ya kuhabarisha na kuelimisha umma mijini na Vijijini kuhusu huduma za usafirishaji, akisema kuwa mchango wa wanahabari ni mkubwa katika maendeleo ya taifa.

“Nyinyi ni mabalozi wa kutafuta ukweli. Nawashukuru kwa kufuatilia na kuandika habari zetu kwa weledi na uaminifu,” ameongeza.

Kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa LATRA imekuja wakati mamlaka hiyo ikiendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwa lengo la kuimarisha usafiri wa ardhini nchini kupitia mifumo ya kisasa na inayozingatia haki kwa wadau wote.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy, amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo washiriki huku akimpongeza Mkurugenzi Mkuu kwa usimamizi mzuri katika kudhibiti ajali za barabarani nchini.













0/Post a Comment/Comments