Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dkt. John Kalage, amesema kuwa licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha elimu bado kuna changamoto kubwa zinazohitaji msukumo wa kifedha ili kutatuliwa kwa ufanisi.
“Tunaitaka Serikali iweke kipaumbele cha kweli kwenye elimu. Ongezeko hili la bajeti litaongeza fursa za upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wote na kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji,” ameema Dkt. Kalage.
Dkt. Kalage amebainisha maeneo yenye changamoto kubwa kuwa ni pamoja na uhaba wa walimu, miundombinu duni ya shule, upungufu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia, pamoja na changamoto kwa walemavu kupata elimu jumuishi.
Shirika hilo limeitaka Serikali kutumia fursa ya mchakato wa bajeti ya mwaka ujao kuweka msingi imara kwa mustakabali wa elimu nchini, likisisitiza kuwa uwekezaji katika elimu ni uwekezaji kwa maendeleo ya taifa.
Post a Comment