::::::::::::
Kufikia Aprili 2025, jumla ya kampuni za wazawa 2,476 na wataalam wazawa 431 wamejisajili katika mfumo huo ambapo Kampuni 300 zimepata fursa za kuuza bidhaa na kutoa huduma mbalimbali kwenye miradi ya mafuta na gesi asilia.
Serikali imeendelea kuimarisha ushiriki wa Watanzania katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia ambapo kupitia EWURA imeendelea kuhuisha kanzidata za watoa huduma na wataalamu wa ndani katika mfumo wa “Common Qualification System - CQS”. Watanzania wanaweza kujisajili kupitia tovuti ya EWURA www.ewura.go.tz.
#Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/26
Post a Comment