KIDATO CHA SITA KUANZA MITIHANI KESHO, MAANDALIZI YAMEKAMILIKA


           ::::::::::

HABARI Baraza la Mitihani Tanzania NECTA limetangaza kuanza kwa mitihani ya kidato cha Sita na Ualimu inayotarajiwa kuanza Kesho Jumatatu Mei 5.2025 nchi nzima

Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt. Said Mohammed amesema jumla ya watahiniwa 134,390 wamesajiliwa kufanya mtihani huo wa kidato cha sita ambapo watahiniwa wa shule ni 126,957 na watahiniwa wa kijitegemea ni 7,433 huku walimu watakaofanya mtihani ni 10,895

Aidha amesema kuwa maandalizi ya mitihani hiyo yamekamilika huku akitoa wito kwa kamati za mitihani kuhakikisha kuwa usalama wa vituo vya mitihani unaimarishwa na kuhakikisha vituo hivyo vinatumika kwa mujibu wa muongozo uliotolewa na baraza hilo 

Baraza hilo pia limewataka wasimamizi wa mitihani walioteuliwa kuhakikisha kuwa wanasimamia mitihani hiyo kwa weledi na uadilifu wa hali ya juu kwa kuzingatia kanuni na miongozo ya baraza hilo

















0/Post a Comment/Comments