MRADI MPYA WA UDSM NA WHI KULETA MAGEUZI YA KIUCHUMI NA KIJAMII

               ::::::::

CHUO Kikuu cha Dar es salaam UDSM kwa kushirikiana na Watumishi Housing Investment (WHI),wamesaini mkataba wa mkataba wa ujenzi wa kituo cha Biashara cha Hill ilikuongeza ufanisi wa huduma kwa jamii.

Kituo hicho kitakuwa na eneo la kuoshea magari,viwanja vya michezo kwa watoto, ofisi pamoja na eneo la mazoezi ya viungo huku likigharimu kiasi cha Sh milioni 8.3 na utakamilika kwa kipindi cha miezi 18.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam.profesa  WILLIAM ANANGISYE amesema  ujenzi wa jengo hilo litakuwa kitega uchumi kutokana na kuwa na ofisi, maduka na maeneo ya michezo ya watoto.

Kwa upande wake Kaimu Afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya watumishi Housing SEPHANIA SOLOMON amesema matarajio katika kipindi cha miaka kumi na tano jengo hilo litaingia Zaidi ya   shilingi billioni kumi na tano ambapo chuo kikuu itapata asilimia arobaini na Taasisi ya watumishi House itapata asilimia sitini.











0/Post a Comment/Comments