SERIKALI YAJIPANGA KUCHIMBA VISIMA VYA MAJI KARIBU NA MAJOSHO


.................

Na Ester Maile Dodoma 

Serikali kupitia wizara ya mifugo na Uvuvi imejipanga kuanza kuchumba visima vya maji karibu na majosho ili kuweza kurahisisha  upatikanaji wa maji wakati wa kutibu  mifugo .

Ameyaeleza hayo Waziri wa mifugo na uvuvi Dkt Ashatu Kachwamba Kijaji wakati wa mkutano wake na waandishi  wa habari leo jijini Dodoma  katika kueleza mafanikio katika sekta ya mifugo na uvuvi kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. 

Kijaji  amewataka  wafugaji kutenga maeneo ya marisho ilikuepusha migogoro kati  ya wakulima na wafugaji  pia kuacha kufuga kimazowea.

Hata hivyo wizara ya mifugo na uvuvi imejipanga kutoa chanjo kwa mifugo ili kuikinga mifugo na magonjwa mbalimbali ambapo asilimia sabini ya mifugo zinatakiwa kuchanjwa .

Vile vile  amewataka wafugaji kufuga kisasa ili kuendana na soko linavyotaka kwani  tumekuwa tukifuga mbuzi wenye  vichwa vikubwa na siyo Ngo'mbe tunavyofikiria  "Ameyasema Ashatu"


0/Post a Comment/Comments