THRDC WATOA MAJAKETI YA UTAMBULISHO KWA WAANDISHI WA HABARI WA MISA TZ

.........

MISA Tanzania imepokea Press Jackets  toka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) Kwa ajili ya usalama wa waandishi wa habari kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Mratibu wa THRDC Onesmo Olengurumwa- amekabidhi press Jackets hizo Kwa Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bwana Edwin Soko wakati wa mafunzo ya KUWAJENGEA UWEZO  waandishi wa habari kwenye kujua sheria za uchaguzi kwenye hotel ya ukumbi wa Mbezi Garden Jijini Dar es salaam 

Naye Mwenyekiti Edwin Soko ameishukuru THRDC na kusisitiza kuwa , ushirkiano baina ya Taasisi hizo mbili utaendelea kuwepo Kwa lengo la kulinda uhuru wa habari na usalama wa waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu ujao.


 

0/Post a Comment/Comments