......
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Lawrence Tax amesema kuwa serikali ya awamu ya sita imeweza kufanikisha kulinda tunu za taifa kupitia Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma wakati akielezea mafanikio ya Wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne chini ya serikali ya awamu ya sita katika uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan Dkt. Tax ameongeza kuwa serikali imehakikisha Tunu muhimu za Taifa zinalindwa kwa kuimarisha umoja , mshkamano na utulivu
Ameongeza kuwa utulivu na amani vilivyopo nchini haviji tu bali kuna kazi kubwa inafanyika kuhakikisha tunu hizo zinaendelea kulindwa .
Post a Comment